Psalms 99

Mungu Mfalme Mkuu


1 a Bwana anatawala,
mataifa na yatetemeke;
anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,
dunia na itikisike.

2 b Bwana ni mkuu katika Sayuni;
ametukuzwa juu ya mataifa yote.

3 cWanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:
yeye ni mtakatifu!


4 dMfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,
wewe umethibitisha adili;
katika Yakobo umefanya
yaliyo haki na sawa.

5 eMtukuzeni Bwana Mwenyezi Mungu wetu,
na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu.


6 fMusa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,
Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;
walimwita Bwana,
naye aliwajibu.

7 gAlizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;
walizishika sheria zake na amri alizowapa.


8 hEe Bwana, wetu,
ndiwe uliyewajibu,
kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9 Mtukuzeni Bwana Mwenyezi Mungu wetu,
mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,
kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu wetu ni mtakatifu.
Copyright information for SwhKC